Banana adai bado anauza albamu zake zilizopita, kuachia albamu mpya

Msanii kongwe wa muziki, Banana Zorro amesema mashabiki wa muziki wake hawatosheki kwa ‘single’ pekee hivyo anajipanga kuachia albamu mpya hivi karibuni.banana ZoroAkizungumza na muziki4life Jumamosi hii, Banana amesema bado anauza CD za albamu zake zilizopita hali ambayo imfanya aendelee kuachia albamu.
“Soko la albamu bado lipo kusema kweli, mimi bado nauza CD za albamu zangu za zamani. Duniani mashaa wote wanauza albamu zao katika show zao, kwanini sisi tushindwe, hata mimi nafanya hivyo kwenye show zangu na ninauza sana,” alisema Banana.
Aliongeza, “Kwa hiyo kila kitu kinawezekana kama ukiamua kujipanga tu, na ndio maana bado nipo kwenye mpango wa kuachia albamu mpya, kwa sababu mashabiki wangu hawatosheki na single moja,”
Pia Banana alisema kabla ya kuachia albamu yake mpya, ataachia wimbo mpya.

Maoni