Dupy: Nimeamua kuwa kimya kumpisha Fraga

Producer wa Uprise Music, Dupy amesema ameamua kumpisha producer mwenzake, Fraga kuanzia mwaka jana mwishoni hadi mwaka huu akidai kuwa yeye amesikika zaidi siku za nyuma. 1620732_1522558781310336_3983955351497163154_n
Dupy ni mmoja kati ya waandaaji wa muziki wanaofanya vizuri huku tayari akiwa ameshaandaa nyimbo kibao zilihit zikiwemo Walalahoi na Kidawa za Izzo Bizness.
“Nimeamua kumwachia Fraga mwaka huu aonyeshe kipaji chake,” Dupy ameiambia muziki4life
 Fraga ndiye aliyeshiriki kutengeneza wimbo wa Harmonize na Diamond, Bado.
“Mwaka juzi na mwaka jana kwa Uprise Music nilikuwa ninasikika peke yangu wakati tupo waandaaji wawili. Mwaka huu nimeamua kumuachia Fraga na yeye aonyeshe uwezo wake. Sitakaa kimya kabisa nitaachia nyimbo chache kama nilivyoanza na ‘Usiji Overdose’ ya Izzo Business na baada ya muda nitaachia wimbo mpya wa Nuh Mziwanda,” aliongeza.
“Lakini nimeathirika kutokana na watu wengi wameshindwa kusikia ladha ya mikono yangu mara kwa mara kama walivyozoea hapo mwanzo.”

Maoni