Kleyah apigana vikumbo na vigogo kwenye chati ya Afrika ya Soundcity

Kleyah anakula sahani moja na wasanii vigogo kwenye chati za Africa Rox Countdown za kituo cha     runinga cha Nigeria, Soundcity.
                    
Wiki hii wimbo wake ‘African Drum’ umekamata nafasi ya tano kwenye chati hizo zinazoangaza video bora za muziki barani Afrika. 
                   Video ya wimbo huo uliotayarishwa na Nahreel imeongozwa na Justin Campos.
Wasanii wengine wa Tanzania waliopo kwenye chati hizo ni Vanessa Mdee, Diamond na Ben Pol.

Maoni