Meneja wa Q Chief na MB Dog, QS Mhonda, amesema tayari ameshafanya mazungumzo na wadau mbalimbali wa muziki ili kulirudisha soko la albamu nchini.
QS Mhonda (kulia) akimkabidhi mkataba director wa video Abby Kazi.
Akizungumza na chanzo chetu Jumamosi hii, mkurugenzi huyo wa label ya QS Mhonda Entertainment, amesema mpaka sasa mambo yanaenda vizuri kuhusu project hiyo.
“Soko la albamu ndio kila kitu kwenye maisha ya wasanii, tukiweza kulirudisha upya hata maisha ya wasanii yatabadilika, kwa hiyo mimi binafsi nipo kwenye mchakato wa kulirudisha upya,” alisema QS Mhonda.
Aliongeza, “Kusema kweli sasa hivi nipo kwenye mazungumzo na baadhi ya watu ili kujua mchakato nzima utakuwaje, lakini tunashukuru Mungu mambo yanaenda vizuri. Kwa hiyo mpango ukikamilika nadhani ndio nitaweka zaidi wazi jinsi itakavyokuwa,”
QS Mhonda amedai mpaka sasa tayari ameshatumia zaidi ya bilioni 1 kwenye muziki katika hatua za kusaidia wasanii mbalimbali.
Maoni
Chapisha Maoni