Mr Blue asema hakutaka watu wajue kama amefunga ndoa

Msanii mkongwe wa muziki, Mr Blue amesema hakutaka kutangaza kama anafunga ndoa kwa kuwa anaamini yale ni maisha yake ya ndani.
Mr Blue akiwa na familia yake baada ya 
kufunga ndoa

Rapa huyo wiki iliyopita aliwashangaza mashabiki wake baada ya kufunga ndoa kimya kimya na mzazi mwenzie Waheeda.
Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii akiwa ‘Honey Moon’, Zanzibar, Mr Blue amefunguka mambo mengi kuhusu ndoa hiyo.
“Ndoa imepita salama kabisa na sasa hivi nipo Honey Moon Zanzibar,” alisema Blue. “Sikutaka watu wajue kama nafunga ndoa kwa sababu ni maisha yangu ya ndani, lakini kwa sababu niliwaalika marafiki zangu, wao ndio walianza kupost picha, sasa baada ya kuona watu wamepost na mimi nikaamua kuweka wazi kilichotokea, lakini kwa yote namshukuru Mungu, pia nimepokea pongezi nyingi sana,”
Katika hatua nyingine Mr Blue amesema akitoka ‘Honey Moon’ ataachia kazi yake mpya na Ali Kiba

   Jiunge nasi Music4life.blogspot

Maoni