Mr Blue asema ndoa haiwezi kumfelisha kwenye muziki

Msanii wa muziki Mr Blue amesema ndoa haiwezi kumsabisha ashuke kimuziki kama baadhi ya watu wanavyofikiria.
blue (1)
Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television, Mr Blue alisema wasanii wengi wakubwa wa Marekani wamefanikiwa licha ya kuwa kwenye ndoa.
“Mimi siwezi kufeli kwenye muziki nimepata mitihani mingi kwenye muziki lakini sijashuka hadi leo, nimeanza muziki nikiwa mtoto na sasa hivi nimeshapata mtoto bado nipo kwenye muziki,” alisema
Aliongeza,”Muziki ni kazi wapo wasanii wengi wa Marekani wameoa lakini wanafanya vizuri, kwa Tanzania mfano Mzee Yusuf ameoa mara mbili lakini sio kwamba ameshuka kwenye game kwa hiyo habari hizi siyo za kweli kabisa”
Mr. Blue amefunga ndoa hivi karibuni jijini Dar es salaam ambapo kwa sasa ana watoto wawili.

Maoni