Wanasema ota ndoto kubwa. Kwa Bright ndoto yake ni kuja kumuoa Vanessa Mdee
Bright (katikati)
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio jana wakati akitambulisha wimbo wake mpya ‘Nitunzie’ aliomshirikisha Barakah Da Prince, Bright ambaye jina lake halisi ni Rashid Said alisema kuwa hajali kuwa Vee Money yupo na Jux kwa sasa.
Kauli ya Bright iligeuka kuwa ‘komedi’ kwa watangazaji wa show hiyo. “Hapana msicheke kwasababu ni kitu ambacho naongea nipo serious kabisa,” alisema Bright.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio jana wakati akitambulisha wimbo wake mpya ‘Nitunzie’ aliomshirikisha Barakah Da Prince, Bright ambaye jina lake halisi ni Rashid Said alisema kuwa hajali kuwa Vee Money yupo na Jux kwa sasa.
“Nataka kumuoa, Vee Money ni mwanamke mzuri kwanza, ni mwanamke mwenye mvuto ambao mwanaume yeyote aliye kamili lazima avutiwe naye.”
Bright amesema anajipanga kutupa ndoano yake kumnasa mrembo huyu. “Hata kama Jux yuko naye, hawajaoana wale, kwahiyo mimi nina nafasi pia ya kuweza kumuambia,” alisisitiza.
Maoni
Chapisha Maoni