Nuh kuachia wimbo ‘Jike Shupa’ akiwa na Ali Kiba

Msanii Nuh Mziwanda ambaye alikuwa akitoka kimapenzi na Shilole kabla ya kuachana amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye hataki kuongea jambo lolote ila mambo yote ambayo yanamsumbua moyoni mwake ameyaongea kupitia wimbo wake mpya uitwao ‘Jike Shupa’.Nuh-na-ShishiMuimbaji huyo amekuwa akilalamika kuwa Shilole alikuwa na mipango ya kutaka kumkwamisha kimuziki kwa kumuwekea vizingiti mbalimbali.
Akizungumza katika kipindi cha East Africa Radio, Nuh amesema sasa hivi hataki tena kuongea mambo ya mpenzi wake huyo kwa kuwa na wimbo maalum wa kuzungumzia swala hilo.
“Mimi siongei mengi kwa sasa wimbo ‘Jike Shupa’ ambao nimemshirikisha Alikiba, utaongea yaliyo moyoni mwangu,” alisema Nuh.

Jiunge na muziki4life.blogspot.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town!

Maoni