Paul Okoye na kofia ya WCB, video ya Diamond f/ P-Square inapikwa?

Ukimuona Paul Okoye wa kundi la P-Square akiwa amevaa kofia ya WCB na yupo Johannesburg, Afrika Kusini ambako Diamond yupo huko tangu mwanzoni mwa wiki hii kuzindua video ya Colors of Africa, ujue mambo yameiva.12599481_945729638858866_1558025152_nPaul amepost picha Instagram akiwa amevaa kofia nyeupe ya WCB, label ya Diamond na kuashiria kuwa huenda wiki hii wakali hao wakashoot video ya collabo yao. Diamond aliingia studio na P-Square mwaka jana.
Kituo cha runinga cha MTV Base kiliripoti wiki hii kuwa Diamond atashoot video ya wimbo huo hivi karibuni.

Maoni