Gari moja limezama baharini eneo la Kivukoni lilipokuwa limeegeshwa likisubiria kivuko.
Inasemekena kuwa gari hilo lilikuwa na abiria wawili wakati likizama. Hadi hivi sasa mtu mmoja (Mwanaume) amekwishapatikana kwani wakati gari linazama aliruka nje ya gari.
Harakati za Waokoaji kutafuta mwili wa pili (mwanamke) zinaendelea na inahisiwa yupo ndani ya gari. Hadi sasa gari halijaonekana.
Maoni
Chapisha Maoni