Tanzania kuna location kibao za video – Malaika

Muimbaji wa ‘Zogo’, Malaika anaamini kuwa Tanzania imebarikiwa mandhari ya kuvutia kufanya video kiasi ambacho si lazima wasanii wapigane vikumbo South.
Malaika Msanii
Malaika ambaye hivi karibuni aliachia wimbo mpya ‘Raruararua’ aliiambia Times FM kuwa bado hajafikiria kwenda kurekodi video nje ya nchi kwa sasa kwa kuwa Tanzania bado kuna Location za kutosha.

“Sioni sababu za kwenda nje ya nchi wakati katika hii nchi yangu kuna location nyingi tu na sijazimaliza,” alisema.

“Bado kuna madirector wengi wenye vipaji nahitaji kufanya nao kazi, yaani kwa sasa bado sijafikiria kwenda kufanya video nje,” alisisitiza.

Jiunge na muzik4life.blogspot.com sasa


Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga

Maoni