Wimbo wa Rama Dee ‘Kipenda Roho’ umeanza kumpa dili mtayarishaji wake, Elly da Bway ambaye amekuwa ni mmoja kati ya waandaaji wa muziki watakaokuja kufanya vizuri hapo baadae.
‘Kipenda Roho’ ni miongoni mwa nyimbo zinazofanya vizuri kwa sasa kwenye media na hata hivyo uwavutia masataa wengi baada ya siku kadhaa zilizopita, Idris Sultan alipost kipande cha video akiusikiliza wimbo huo kwa hisia na kuandika, “Rama Dee Kipenda Roho aiseeee hii nyimbo ni habari nyingine unaweza mrudia ex wako wa 1970 wakati umezaliwa 80.”
Akizungumza na #MZhot, mtayarishaji wa wimbo huo Eliudi Kipimo maarufu kama Elly da Bway, alisema, ‘nashukuru wimbo wa ‘Kipebda Roho’ umeanza kunipa dili na mastaa’.
“Nimefanikiwa kufanya nyimbo nyingi lakini huu ‘Kipenda Roho’ ni wabahati kwangu. Mastaa wengi wameanza kunitafuta ili tufanye kazi. Jux ni mtu wa kwanza kuomba tufanye kazi baada ya kuusikia wimbo huo tuliupoonana,” aliongezea.
Elly da Bway amewahi kufanya kazi na wasanii wengi wakubwa akiwemo, Rama Dee, Alikiba, Lady Jaydee na wengine wengi.
Maoni
Chapisha Maoni