Jifunze Hapa ifanye simu yako ya Android kuwa na sauti nzuri

Njia mbadala zinazoweza kuongeza ubora wa sauti katika simu yako ya Android
1. Angalia katika settings (mipangilio) ya simu yako Sound Enhancement Settings
Simu nyingi huwa zinakuja na sehemu maalumu ya kuset kiwango bora cha sauti katika sehemu
ya settings na kubadili kabisa uwezo wa simu yako katika kutoa na kupoke mawimbi ya sauti.
Kwa simu za HTC nenda kwenye BoomSound na hapo utaweza kuset vizuri
mipangilio yako ya sauti na kwa wale wenye M Series wanaweza wakaenda kwenye Beat Audio.
Kwa watumiaji wa Xperia wao wanaweza kutumia ClearAudio ambayo inapatikana kama application ya peke yake au kwenye settings. Clear Audio ina Equalizer ambayo itakuwezesha kuset ubora wa sauti unaotaka.
Kwa watumiaji wa Samsung wanachotakiwa kufanya ni kuchomeka earphone au spika ya nje,
alafu utaend kwenye settings, alafu utaenda mpaka kwenye sound, hapo utaweza kuset ubora wa sauti unaotaka wewe.
                       Music-Volume-EQ-android 

2. Pakua Application bora ya kusikilizia miziki (Best Music Players Apps)

Kama simu yako haina sehemu ya kurekebishia ubora wa sauti unashauriwa kupakua baadhi ya application bora zaidi za kusikilizia muziki ambazo zina uwezo mkubwa wa kuset ubora wa sauti kama vile Poweramp ,n7player na Equalizer+. Kwa wale wanaopenda kuangalia video kwenye simu au tablet zao wanaweza wakapakua VLC.

3. Pakua Application bora kabisa ya Equailizer

Application nyingi za kusikilizia muziki hazina uwezo wa kuboresha sauti inayotoka kwenye simu tofauti na ile ya muziki unaopigwa. Hivyo ni bora kupakua application itakayokuwezesha kuset ubora wa sauti hata ule wa kuongea wakati unapopiga simu. Hapa unashauriwa kuingia playstore na kupakua applications kama Music Volume EQ na Bass Booster.

4. Nunua headphones au earphones zenye ubora

Haina maana ya kuset ubora wa sauti katika simu yako kama una arphones ambazo ubora wake ni wa kiwango cha chini. Hapa unashauriwa kununua earphones zenye uwezo wa hali ya juu wa kutoa sauti kama wakati unaposikiliza muziki wako. Kama wewe ni mpenzi wa muziki usijali sana bei ya earphone jaribu kununua ile itakayofaa kwa matumizi yako, pia itasaidia sana kupunguza uharibifu wa masikio yako.

5. Njia mbadala

Kuna njia nyingine nyingi kama kuifanya spika yako kutoa kiasi cha mwisho zaidi cha sauti kwa kuinstall application ya AudioFX, hii inahitaji simu iliyorootiwa. Pia unaweza ukaangalia kama kava lako la simu linazuia kipini cha earphone kisiingie vizuri katika tundu lake au spika isitoe vizuri sauti.
MAWASILIANO Yangu ni kwa  
Simu piga  +255787856122 au
Email  jellymilazo@gmail.com

Maoni